Baada ya kimya kirefu cha katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (chadema),Dr Wilbroad Slaa juu ya kashfa ya kujikopesha pesa huku ikichukuliwa kama ni njia ya kukihujumu chama hicho amewaambia watanzania kuwa wayabeze malalamiko hayo kwa ni hayana ukweli wowote.
"Hoja ya kujikopesha kwa sura ya ufisadi ni "mfu" nimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine. Aidha siyo 140 Million. Zote milioni 20 zililipwa awamu ya mwisho June 2012. Hivyo hakuna deni la chama tena.
2. Josephine hajawahi kulipwa hata senti mmoja na chama kwa ziara za Mikoani, wala kwa shughuli yeyote ile isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3" alisema Dr slaa.
Taarifa hizi zilianza kuvuma na kutawala vyombo vingi vya habari baada ya wanachama waliojulikana kama watovu wa nidhamu kufukuzwa katika chama hicho(masalia)
No comments:
Post a Comment