![]()
MSAJILI wa vyama vya Siasa, John Tendwa, ameibua mjadala mzito kwa viongozi wa vyama vya upinzani ambao wamemtaka kuwaeleza Watanzania kama anamiliki kadi yoyote ya chama cha siasa, kabla ya kuhojiwa kwenye Baraza la Vyama vya Siasa.
Mjadala huo umeibuka jana,ikiwa ni siku moja baada ya Tendwa kutoa tahadhari kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa kinapaswa
kuhakikisha kinasimamisha mgombea urais mwaka 2015,anayekubalika kwa Watanzania na kuhimili nguvu za wapinzani.
Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, viongozi wa vyama vya upinzani walimshambulia Tendwa na kusema amejiingiza kwenye itikadi za CCM na kusahau jukumu la kusimamia sheria za usajiri wa vyama na kuvilea bila upendeleo.
NCCR–MAGEUZI: Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, amemtaka Tendwa kuwaeleza viongozi wa vyama vya upinzani jinsi ya kufanya ili kushika dola kama alivyoishauri CCM.
“Sasa Tendwa amevuka mipaka,yeye anatakiwa awe juu ya vyama vya siasa, lakini jana (juzi),imejidhihirisha yuko chini ya itikadi ya CCM.
“Nikiwa Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), tunamtaka avieleze vyama vya upinzani ofisi yake, inaendeshwa kwa itikadi ya chama gani na mfumo gani anaotumia kutimiza majukumu yake.
“Tatizo kubwa tulilonalo ni mfumo wa katiba iliyopo sasa ndio inampa uhuru hadi kutamka kauli kama hiyo, kwani ikichunguza kwa
makini utagundua tupo katika mfumo wa chama kimoja tawala ingawa kuna vyama vingi,” alisema.
AFP: Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima (AFP), Rashid Rai,alisema ameshtushwa na kauli ya Tendwa kutoa ushauri kwa CCM juu ya kumteua mgombea anayekubalika kwa Watanzania.
“Hili ni jambo kubwa, Tendwa amekurupuka na ameonyesha wazi ana mapenzi na CCM, hili ni kama askari wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), kupiga picha na viongozi wa siasa, akiwa na sare zake.
“Sasa suala hili, tunataka tulifikishe kwenye baraza letu ambalo linatarajia kukaa Februari mwaka huu, ikiwa hatakuwa tayari kuvishauri vyama vingine.
“Nikiwa kama mjumbe nitalifikisha kwenye baraza na Tendwa ataitwa kuhojiwa kwenye kikao,” alisema.
CUF: Naibu Katibu Mkuu Bara CUF,Julius Mtatiro, alisema kauli ya Tendwa imedhihirisha anamiliki kadi ya CCM ambayo imekuwa ikimsababisha kutoa kauli tata za kutetea chama hicho.
“Tendwa tunamjua yeye ni kada wa CCM na hata kadi inawezekana anayo ameificha, yupo pale kwa ajili ya chama tawala, sasa kauli
yake hii bila shaka ameitoa kwa kujisahahu kwa sababu ya ukada.
“Ni vema akaviachie vyama vifanye siasa zake yeye abaki kusimamia usajili, kanuni na ulezi na sio kutetea chama kimoja,kwanza tunamshangaa kukimbilia mambo mepesi wakati upinzani tunapigwa na polisi kwenye kampeni hasemi chochote.
“Tumekuwa tukinyang’anywa waziwazi ushindi wa majimbo na kata lakini anakaa kimya, iweje leo anaibuka kwenye mambo rahisi
yanayoleta chuki,” alisema.
CHADEMA: Kwa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewataka Watanzania kutambua kuwa Tendwa ni adui mkubwa wa demokrasia.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, ilisema Tendwa amekuwa akitumiwa na CCM ili kufanikisha malengo yao.
“CHADEMA tunasema, Tendwa ni mchezaji wa benchi la CCM na amekuwa akitumia ofisi yake kutimiza azma ya chama tawala kwa kupitia mlango wa nyuma, sasa tunasema pamoja na kauli yake haituzuii kutimiza malengo yetu.
“Mara zote, Tendwa yupo ofisini kwake kwa ajili ya kukishughulikia CHADEMA na kutoa vitisho, sasa tunamwagiza akawaeleze CCM
mwaka 2015 watapotea kwenye siasa kama Chama cha KANU cha nchini Kenya,” ilisema taarifa hiyo.
CCM: Wakati vyama vya upinzani vikipinga vikali ushauri huo, CCM kimempongeza kwa ushauri wake.Akizungumza na MTANZANIA Dar
es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye,alisema tahadhari iliyotolewa na Tendwa itafanyiwa kazi kwa kuwa
ni mzuri na una manufaa makubwa ndani ya chama na taifa kwa ujumla.
“Tumepokea ushauri huo ambao ni kama tahadhari kwetu, kwani yeye ni msajili wa vyama vya siasa na hiyo ni tathmini yake aliyoiona na kuamua kusema pia ana uhuru wa kushauri chama chochote kwa kuwa anayo mamlaka hayo.
“Kwa upande wetu, CCM tumepokea kwa mikono miwili na tunasema ametoa mapema na wakati muafaka ili kuyafanyia kazi kama alivyosema kwamba tujitafakari tulipotoka, tulipo sasa na tuendako,” alisema.
Juzi Tendwa alinukuliwa na vyombo ya habari akitoa tahadhari kwa CCM kusimamisha mgombea urais mwaka 2015 anayekubalika, ili kukabiliana nakuhimili nguvu za vyama vya upinzani.
Article 18 [a] Every person has a freedom of opinion and expression of his ideas (United Republic of Tanzania Constitution)
Edwin Bliss C
Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.
Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.
Friday, January 11, 2013
VYAMA VYA UPINZANI VYAMJIA JUU TENDWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment