Mkurugenzi aigomea bodi ya CCM kujiuzulu.
15.7.2013
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamapuni ya Peoples Media Communication ilio chini ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mikidadi Mamhomud amekataa kujiuzuu wadhifa wake mbele ya wajumbe wa Bodi ya Uhuru FM katika kikao kichoongozwa na kigogi wa ccm imefamika.
Habari za uhakika toka miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho zilipatikana mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho zimeeleza kuwa wajumbe kwa pamoja hawakuridhishwa na utendaji wa Mkurugenzi huyo na kuifanya Uhuru FM inayomilikiwa na CCM kuzorota.
Kutokana na kusuasua kwa utendaji wa Radio hiyo na kumalizika kwa mkataba wa Mkurugenzi huyo toka mwaka 2010 , wajumbe walipendekeza ajiuzulu ili kutoa nafasi kwa watu wengine kuomba nafasi hiyo.
Mambo kadhaa yameelezwa na wajumbe yakimuelemea Mikidadi ambaye ni mtangazaji wa siku nyingi wa Radio Tanzania Dar es Salaam,Radio one na ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam kwa kipindi kimoja.alishindwa kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo ya uenyekiti wa ccm wilaya ya ilala kutokana na ubadhilifu wa fedha na mali za chama alioufanya kipindi alichopata uenyekiti huo,na tabia hii ya ubadhilifu ameiendeleza hata alipopewa ukurugenzi wa Radio uhuru.
Mjadala mkubwa ndani ya kikao hicho ulitokana na kufanyika kwa tathmini ya utendaji na ufanisi wa Radio hiyo ,hali iliothibiitika kuwa imepoteza kundi la wasikilizaji na kukosekana kwa mvuto kwa wasikilizaji na pia kukosekana kwa ari ya wafanyakazi ambao hutayarisha vipindi na kupiga debe ili kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kushinda kwenye chaguzi zake kuu.
Hata hivyo kwa upande mwingine malalamiko ya msingi toka kwa wafanyakazi wa kituo hicho ni juu ya makato ya fedha ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) kudaiwa kutowasilishwa kunakohusikili hali fedha ya wafanyakazi inakatwa kila mwezi na pia baadahi ya wafanyakazi kudai kuna ubadhirifu mkubwa wa fedha za taaasi na mali zake.pia kuna tuhuma za tasisi hiyo kutolipa kodi(PAYEE) TRA ili hali wafanyakazi wanakatwa kodi hiyo kila mwezi.
Pia kuna madeni makubwa sana yanayoikumba tasisi hiyo ambayo nayo yametokana na ubadhilifu huo wa fedha za tasisi.baadhi ya madeni yanayoikabili tasisi hiyo mbali na NSSF,TRA, ni deni kubwa la pango la minara ya kurushia matangazo huko Kisarawe, Mbeya, Dodoma , Tabora, Tanga na Arusha na Mwanza, kituo kinapata matangazo ya biashara,fedha za malipo hazionekani ,hili limetukera kama wajumbe wa bodi tunataka hatua zichukuliwe ”Alisema mmoja wa wajumbe wa Bodi hiyo.
Aidha mjumbe mwingine alisema kikao hicho cha wajumbe wa bodi kimepata taarifa za kutosha toka kwa wadau mbali mbali kuwa Mkurugenzi huyo amekuwa akiajiri ovyo ovyo wafanyakazi wasio na sifa wala uwezo kwa njia za kujuana,undugu na upendeleo badala ya kubaki na timu ndogo itakayolipwa mishahara mizuri. mfano amemuajili mwanae wa kumzaa(ABDUL MIKIDADI) katika Redio hiyo bila hata ya kufuata taratibu za ajira zinazostahili., hana sifa wala elimu yoyote wakati wapo vijana wasomi wengi tu wapo mitaani wanahainga kutafuta kazi.ameajili vijana ambao ni watoto wa majirani zake huko anakoishi bila ya kuzingatia taratibu za ajira.hawana sifa yoyote.hii yote ni ajira za kujuana tu.
Jambo jingine lililoelezwa na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo ya Radio ya CCM ni kutosikika kwa matangazo katika masafa yake kwenye Mikoa ya Arusha,Tanga na Tabora kwa muda mrefu huku uongozi chini ya Mikidad ukikataa kuchukua hatua.
Kwa upande mwingine taarifa zinaeleza kuwa tayari bodi hiyo ilishampeleka mshauri mwelekez katika kituo hicho na kutaka yafanyike maboresho pamoja na kupunguzwa kwa baadhi ya wafanyakazi ambao hawana tija na sifa ya kiutendaji.
Taarifa za uhakika zimebainisha kuwa lawama kubwa anatupiwa mkurugenzi aliyepo kwa kushindwa kuhimili ushindani na vyombo binafsi licha ya Uhuru FM kuanzishwa mwaka 2000 lakini hadi sasa ikikosa hadhi na kushuka chati.
"Wafanyakazi wa Radio yetu si wakoofi ila ni jasiri, hawataki kuonewa na kuburuzwa, hutumia akili na maarifa katika kujituma lakini wanakatishwa tamaa hasa katika malipo ya posho, mishahara ya upendeleo kwa wengine kulipwa mishahara kiduchu bila ya kuangalia utendajikazi wa mtu au elimu yake.
Kitendo cha mkurugenzi huyo (mikidad) kukataa kujiuzuru nafasi hiyo na hasa kutokana na tuhuma zinazomkabili ,tuhuma za Ubadhilifu wa fedha na mali za tasisi hiyo, tuhuma ya ngono kwa wasichana wanaotaka ajira katika redio hiyo,ajira za upendeleo na undugu,mishahara ya upendeleo nk ,kitendo hicho kinatafusiliwa kuwa huenda labda urafiki wake na katibu mkuu wa CCM ndio unampa kiburi na jeuri hiyo ya kutojiuzuru.
Mwisho kama kweli ile sera ya kuvua gamba ipo active,basi hili ni gamba lingine linalopaswa kuvuliwa haraka kabla mambo makubwa na ya hatari hayatokea katika tasisi hii zaidi ya kesi iliyopo mahakamani kwa sasa ya ubadhilifu wa fedha za wafanyakazi za NSSF inayomkabili mkurugenzi huyu .
HAYA SI MAJUNGU BALI NI UKWELI AMBAO NIMEULETA HAPA ILI UMMA UYAJUWE NA KUYAELEWA.
No comments:
Post a Comment