Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Saturday, December 7, 2013

ASHA -ROSE MIGIRO, NAPE MNAUYE, KINANA WAFUNZWA ADABU



Leo katika jimbo la Spika wa Bunge la Tanzania Anna Makinda imetokea sintofahamu kubwa sana hasa katika kipindi hiki ambacho tume ya taifa imetanzaza chaguzi za nafasi zilizoachwa wazi taifa zima ambao utafanyika 9- feb mwakani.


Eng Rwenge, Jar People, Asha- Rose Migiro, Nape Mnauye pamoja na mzee wa Tembo walilundikana jimboni hapa ikiwa ni maandalizi ya kupima upepo juu nani ni nani katika uchaguzi ujao wa kiti cha udiwani katika kata ya njombe mjini.


Mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya kanisa katoliki( pale ilipotua helkopta wakati wa ujio wa mh mbowe na tundu lisu) ulianza saa tisa  na kuisha saa 11 kasoro hivi umekuwa wa  kihistoria mkoani njombe ukizingatia ndiko anakotoka mh spika na ni katikati ya mji wa njombe.

Pamoja na juhudi za kusomba watu maeneo mbalimbali vijijini lakini hali ilikuwa tete tangu wanaanza mpaka wanamaliza.


NAPE MNAUYE AKURUPUA MATUSI KWA CHADEMA

Sijui kama ni kuchanganyikiwa ama vipi lakini katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi ameshindwa kuzungumza hoja kwa wananchi zaidi ya matusi na kejeli kwa Chadema, hii imepelekea hata wachache waliokuwepo kuanza kuondoka kwenye eneo la tukio kwa madai hakuna cha maana wanachokipata.

WATENDAJI NAO WANENA.

katika pitapita zangu hapa na pale nikakutana na watendaji wanaofahamu kuwa mimi ni Chadema, hawakusita kuniambia mipango iliyo ndani ya chama cha mapinduzi baada ya kunihakikishia kuwa waliitwa kwenye kikao na viongozi wa ccm wakisisitiziwa kukiunga mkono chama chao ili kuzilinda ajira zao jambo ambalo lilipingwa vikali na baadhi ya watendaji hao hivyo kuhatarisha vibarua vyao.

MAONI YA WANANCHI

sehemu kubwa ya wananchi inawashangaa viongozi wa CCM kwa kuendeleza propaganda bila ya kutatua matatizo yanayowakabili mda mrefu hususani upatikanaji wa maji. hii imewapelekea kuwa bize na shughuli zao bila kujali nani alikuwepo kwenye ardhi yao kwa muda huo, katika maongezi yao wameahidi kuwaumbua ccm kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani

.Baadhi ya picha za mkutano huo




MZEE KINANA AKISEMA YA MOYONI

SAFU YA UONGOZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI NA WAANDISHI WA HABARI




WACHEZA SHOO KATIKATI WAKIMCHEZEA KINANA

SEHEMU YA WANANCHI WAKIMSIKILIZA KINANA

WENGINE WAKIONDOKA BAADA YA NAPE KUANZA MATUSI

SOURCE
THE MAYEMBA BLOG

No comments:

Post a Comment