Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Sunday, February 9, 2014

NJOMBE:MH SILINDE AFANYA KUFURU, CCM WAKIMBILIA POLISI




Ni katika mkutano wa mwisho wa kufungia kampeni za kumsaka diwani wa kata ya Njombe mjini katika jimbo la Njombe Kusini ambalo kwa sasa linaongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama ANNA MAKINDA.


Mh Silinde ambaye ni mbunge wa jimbo la Mbozi Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia ndiye aliyepewa dhamana ya kuhakikishwa ushindi unapatikana kata katika kata hiyo
aliongoza maandamano makubwa yaliyokuwa na msisimko na mwamko mkubwa sana.

Maandamano hayo  yaliyofanyika huku mvua kubwa ikinyesha yalihudhuriwa na wakazi maelfu kwa maelfu wa kata ya njombe mjini.

Hii ilipelekea chama cha mapinduzi kushindwa kabisa kufanya mkutano wao hivyo kukimbilia polisi kuomba msaada ili kusitisha zoezi la msafara wa CHADEMA.\

Haikufua dafu kwani viongozi walijipanga vizuri na waliwashinda polisi kwa hoja na kuendelea na msafara wao huku polisi wakighairi na kuanza kulinda msafara huo.

Hivi ndivyo ilivyokuwa leo katika picha



Polisi walipovamia msafara wa CHADEMA

wananchi wa kata ya njombe mjini wakishangilia bila kujali mvua iliyokuwa inatiririka bila kikomo.






viongozi na wanachama wakiwa mbele ya msafara wa magari kuelekea uwanjani kufunga kampeni








No comments:

Post a Comment