Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Monday, December 31, 2012

ASKARI ALIYEPIGA PICHA NA LEMA ATOROKA


JESHI la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), limesema askari anayedaiwa kuwa jeshi hilo aliyepiga pichaMbunge wa Arusha Mjini (Chadema), GodblessLema ametoroka.


Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema jana kwamba pamoja na hatua yake
ya kutoroka, jeshi litaendelea kumsaka kwa udi na uvumba ilikumhoji na kujiridhisha kama
kweli ni mwanajeshi wake kabla ya kumchukulia hatua zakinidhamu kwa mujibu wa
Kifungu cha 147 cha Katiba ya Jamhuri wa Muungano waTanzania ya 1977.


“Huyu kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini wakati
tunaendelea na uchunguzi alitoroka katika nyumba aliyokuwa amepanga bila ya
taarifa kwa baba mwenye nyumba,” alisema Kanali Mgawena kuongeza.


“Askari huyo alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga mita chache karibu na Kituo cha Polisi
cha Simanjiro, Arusha na alikuwa akijishirikisha na ulinzi shirikishi.”
Alipoulizwa jina la askari huyo,Kanali Mgawe alijibu: “Yeye alikuwa anafahamika mtaani
 hapo kwa jina la kamanda.” Hata hivyo, Kanali Mgawe alisema jeshi hilo litahakikisha linatoa
ripoti kamili kwa umma baada ya kumkamata na uchunguzi kukamilika ili kuondoa utata
uliogubika suala hilo.

 Alipoulizwa kama kuna tofauti gani kati ya mwanajeshi kuingia
kwenye mikutano ya wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kisiasa kama wakuu wa wilaya
na mikoa, Kanali Mgawe alijibu:” Wanajeshi wanaofanya kazi za U- DC au RC, wanaruhusiwa
kisheria.”Alifafanua kuwa iwapo mwanajeshi atateuliwa kufanyakazi katika taasisi yeyote ya
Serikali nje ya jeshi, atatakiwa kuvua magwanda ya jeshi na  kufanya kazi hiyo mpaka
atakapomaliza muda wake na baada ya hapo ataruhusiwa kurejea jeshini.


“Kuna kitu kinaitwa ‘secondment.’ Mwanajeshi anaruhusiwa kufanya shughuli
zozote nje ya jeshi iwapo atahitajika kufanya hivyo. Ila kwa masharti ya kuvua magwanda,
hivyo wananchi wasishangae kuwaona baadhi ya askari wetu ni wakuu wa wilaya na mikoa na
baadaye kurudi jeshini kuendelea na majukumu yao,” alisema Kanali Mgawe na
kuongeza: “Askari akiwa katika majukumu yake mapya, atafanya kazi zote
atakazopewa zikiwamo za kisiasa kama ilivyo kwa wakuu wa wilaya na mikoa, lakini
akirudi jeshini, anarudi kuwa askari mwenye utii na kufuata kanuni za jeshi zisizofungamana
na siasa.”

(Chanzo gazeti la Mwananchi)



 

No comments:

Post a Comment