Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Monday, December 31, 2012

MAANDAMANO MTWARA YAMEIKOSESHA SERIKALI USINGIZI


Katika Hali ya Kuweweseka kuhusu maandamano yaliyofanyika juzi Mtwara Kupinga usafirishaji wa gesi asilia kwenda Dar. Waziri Sospeter amesema Wanasiasa ndio walio ratibu maandamano kwa nia ya kutaka nchi igawanyike vipandevipande.

Amedai Gesi ni ya wa Tanzania na sio wana Mtwara peke yao kwani hata wakiachiwa hawataweza kuitumia. Amewaambia wanaoratibu Maandamano kuwa Mbona wakati gesi haijagunduliwa Wana Mtwara walikuwa wanafaidika na fedha zinazo tokana na Mkonge Morogoro Na Tanga?? Alipoulizwa kuhusu hatua walizo wachukulia wanasiasa hao alisema yeye na wizara yake hawahusiki kuchukua hatua.

Amesema pia anaandaa taarifa ambayo itaelezea kinagaubaga jinsi wanasiasa walivyoratibu maandamano na ataitoa baada ya Tamko la serikali litakalo tolewa na Raisi leo atakapo kuwa anatoa hotuba ya Kufungia mwaka.

Source Radio One

No comments:

Post a Comment