Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Wednesday, December 19, 2012

CHADEMA YAAHIDI KURUDISHA TWIGA HAI WALIOUZWA NA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI

Hayo yamezungumzwa na mbunge wa jimbo la Musoma mjini(Vicent Nyerere) leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa  mjini Iringa

Nyerere amesema watakaporudi bungeni atahakikisha anampa ushirikiano mkubwa mhe msigwa ili serikali irudishe twiga wote waliotoroshewa nje ya nchi kwani hayo ni matumizi mabaya na ya makusudi ya rasilimali ya umma

Mbunge Msigwa ambaye ndiye aliyekuwa mwenyeji wa mkutano huo aliwakumbusha wananchi kuwa nchi haitaweza kuendelea kwa sababu ya tabia na mfumo wa kiutawala wa chama cha mapinduzi
aidha Msigwa ameongeza kuwa uongozi ndani ya ccm unapatikana kwa rushwa majungu na kujipendekeza na kuwa ili uwe kiongozi ndani ya ccm ni lazima uwe ni mnafiki muongo sifa ambazo haziwezi kulivusha taifa kutoka hapa tulipo.

ONA WATU WALIVYOJITOA KULIPIGANIA TAIFA HILI


Baadhi ya viongoziwa chadema Vicent Nyerere kushoto,Peter Msigwa katikati na katibu wa mbunge Nyerere wakimfuatilia mmoja wa wanfunzi wa vyuo vikuu iringa (hayupo pichani)akihutubia mkutano muda mfupi kabla viongozi hao hawajapanda jukwaani

Mweka hazina wa chadema tawi la chuo kikuu cha "ruco" bi Jesca Kishoa akiwahutubia wakazi wa mji wa Iringa (hawapo pichani) katika viwanja vya mwembetogwa leo



Mwenyekiti wa chadema tawi la chuo kikuu cha "ruco" bi Rose Mayemba akiwahutubia wakazi wa mji wa Iringa (hawapo pichani)katika viwanja vya mwembetogwa leo
Mhe Vicent nyerere Mbunge wa musoma mjini akiwahutubia wakazi wa mji wa Iringa(hawapo  pichani)katika viwanja vya mwembetogwa leo

No comments:

Post a Comment