Leo ni takribani wiki mbili tangu kuanza kwa mashindano ya kombe la Mbunge wa iringa mjini Mch Peter Msigwa yanayoendelea katika viwanja mbalimbali hapa manispaa ya iringa mjini
Kutokana na majukumu mengine kitaifa(ikizingatiwa kuwa yeye ni waziri kivuli wa mali asili na utalii) alishindwa kuwa nao kwa kipindi cha wiki nzima tangu kuanza kwa mashindano hayo.
baada ya mhe kurudi jimboni alianza kutembelea viwanja mbalimbali vya michezo kwa ajili ya kuwapa hamasa na kuwatia moyo wachezaji wao
leo Mhe alitembelea viwanja vya michezo kadhaa katika manispaa na ameshangaa kuona namna vijana walivyoyapokea kwa furaha mashindano hayo
Mhe Peter Msigwa akiwapa mawaidha wachezaji wa "ac milan" na" dabaga road" katika viwanja vya kanisani kata ya ruaha kabla hawajaingia kwenye mchuano
".ac milan" na "dabaga road" wakichuana vikali uwanjani
watoto na vijana waliojitokeza wakifuatilia mpira kwa makini
timu ya ac milan ikiwa katika mapumziko baada ya dakika 45 za awali kukatika huku wakiwa na sare ya kutokufungana
Mhe Peter Msigwa akiwa katika pozi na wachezaji wa ac milan(wamevaa sare nyeupe) pamoja na dabaga road(wamevaa sare nyeusi) katika viwanja vya kanisani kata ya ruaha
Mhe Msigwa akifuatilia kwa makini mpira uliokuwa ukichezwa kati ya ac milan na dabaga road
Mpira mlimalizika kwa ac milan kuinyuka timu ya dabaga road magoli 3-1
Hii bado ni raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambayo itafuatiwa na mechi za mtoano
No comments:
Post a Comment