Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Thursday, December 20, 2012

MEYA WA MANISPAA YA IRINGA AMPONZA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA......

Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa mh.Jescar msambatavangu amejikuta katika wakati mgumu katika kikao cha dharura cha baraza la madiwani manispaa ya iringa  baada ya meya wa manispaa hiyo mstahiki Aman Mwamwindi na mkurugenzi wa manispaa ya Iringa bibi Teresia Mahongo kumkaribisha mwenyekiti huyo na kumpa kiti katika meza kuu wakati kikao hicho kikiendelea
 
Taarifa kutoka katika kikao hicho zimeeleza kuwa mh.Jescar ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitanzini  aliingia ukumbini hapo na kwenda moja kwa moja kukaa katika viti vya waheshimiwa madiwani lakini muda siyo mrefu meya Mwamwindi na mkurugenzi wakamwita na kumpa kiti meza kuu
 
Inaelezwa kuwa mara baada ya tukio hilo diwani wa kata ya mivinjeni Frank Nyalusi (chadema)alihoji sababu ya diwani huyo kupewa kiti meza kuu "mstahiki meya nataka kujua sababu ya diwani wa kata ya Miyomboni Kitanzini kukaa kiti cha mbele kwenye kikao hiki cha kiserikali" alihoji Nyalusi.
 
meya Mwamwindi akajibu kuwa diwani huyo amepewa kiti hicho kwakuwa ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa iringa nakuongeza kwamba kwakuwa ilani inayotekelezwa ni ya ccm mwenyekiti huyo ana uhalali wa kukaa meza kuu
 
Inaelezwa kuwa majibu hayo ya meya yalizua zogo na kurushiana maneno baina ya madiwani wa ccm na wale wa chadema huku mbunge wa iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akihoji ni kanuni ipi iliyomruhusu mwenyekiti wa chama kukaa meza kuu katika kikao cha kiserikali
 
Habari zaidi zinaeleza kuwa mara baada ya mchungaji Msigwa kuhoji uhalali huo madiwani wa ccm bila kujali kanuni zinasemaje kuhusiana na suala hilo walidai suala hilo liamuliwe kwa kura wakilenga kumnusuru mwenyekiti wao asiumbuke lakini wakashindwa kwa hoja za madiwani wa chadema na hatimaye mwenyekiti huyo akalazimika kurudi katika viti vya waheshimiwa madiwani    

No comments:

Post a Comment