Baada ya Rais wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete kupingana na maamuzi ya wanamtwara juu ya usafirishwaji wa gesi asilia kutoka mtwara kwenda Dar es laam, na kufanyika kwa vikao mbalimbali vya chama nvinavyopanga namna yaa kuwaadhibu waliopanga maandamano hayo,wananchi wa wamtwara wamekaa jana na kutoa kauli ya mwisho juu ya maamuzi yao
wakizungumza katika kikao hicho wamesema hawataruhusu kwa namna yeyote ile gesi isafirishwe wakati wao waakiendelea kuwa masikini, mmoja wa wahanga hao huku akiwa na hasira kali alisema hawako tayari kuzulumiwa haki yao ya msingi na serikali hiyo na akasisitiza kuwa liwalo na liwe.
Huku sakata hilo likiendelea kuwa na sura mpya Maaskofu nao wameonesha wazi kutokuiunga serikali mkono katika maamuzi yao kwani kwa kufamya hivyo ni kuwaumiza wananchi
Wananchi wa Mtwara wakichangishana pesa za kusaidia harakati za ukombozi
Mmoja kati ya wananchi akizungumza jambo juu ya maamuzi ya Rais Jakaya Kikwete kutokubali gesi kubaki Mtwara


No comments:
Post a Comment