Katika hali ya kushangaza imeonekana
kuwa Rais wa nchi Jakaya Kikwete amekuwa akihudhuria zaidi misiba ya wasanii
nchini lakini si misiba ya watu ambao ni msaada mkubwa kwa taifa hili.
Ukweli ni kwamba kama aliamua kuwa baba
mbona amewabagua watoto namna ya kuwalea
na kuwatunza?mbona ni watumishi wengi wa umma wamekufa tena wengine katika vifo
vibaya na vya udhalilishaji lakini hatukuona mchango wake?
Hebu angalia matukio haya;
Msiba wa Mwangosi wala salamu za
rambirambi hatukusikia!
Amefariki Dkt. Sayi na Prof. Carneiro
wote hawa ndio waliokuwa madakatari bingwa pekee wa upasuaji wa watoto pale
Muhimbili, hatukusikia Rais kahudhuria.
Mwaka 2009 alifariki Profesa Aziz, Daktari
bingwa wa upasuaji pale Muhimbili na aliyetibu watu wengi sana, aliugua na
Serikali ilimwambia hawawezi kumpeleka kwa matibabu, akakopa pesa Agha Khan
Hospital akaenda kutibiwa Ujerumani, aligundulika kuwa ana saratani ambayo alikaa nayo na kuja
kufariki miaka kumi baadae akiwahudumia Watanzania Muhimbili, akufundisha
Madakari wa upasuaji, alifariki na kuzikwa hatukuona wala salamu toka kwa Rais!
4.Tuna wiki tatu sasa amefariki Dkt.
Bashiri aliyekuwa daktari mzuri sanakwa vipimo vya ultrasound,
amehudumia Watanzania wengi, sijasikia Rais anahudhuria.
Wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wanasema
Hivi...
.Huwa anachagua vipi misiba ya
kuhudhuria?
.Hao washauri wake wanatoka katika
kundi lipi katika jamii?
Source jf
No comments:
Post a Comment