| Wananchi wakiwa wamefunga barabara. |
| Walichoma mataili barabara kuu ya Dodoma-Morogoro kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa serikali ya mkoa wa Morogoro kuzungumza nao, jambo ambalo walifanikiwa. |
| Afisa Tabibu wa Zahati ya Dumila Dkt. Mathew Kayunga. Uliofunikwa kwa shuka jeupe, kushoto kwa daktari ni mwili wa marehemu. |
Afisa Tabibu wa Zahati ya Dumila Dr Mathew Kayunga ambaye
alithibitisha kupokea majeruhi saba waliojeruhiwa kwenye vulugu hizo,pia
alithibitihsa kupokea mwili wa marehemu mohamed Msigala majira ya saa 6
mchana wakati vulugu hizo zikiendele kupamba moto eneo hilo la Dumila
Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.
Alipoulizwa kama kifo cha mzee huyo kimetokana na vulugu hizo Daktari
huyo alidai kwamba hawezi kuthibitisha jambo hilo kwa kuwa marehemu
alifikishwa kwenye Zahanati hiyo kwa usafiri wa boda boda akiwa tayari
amekufa.
" Huyu marehemu kaletwa hapa tayari amekufa hivyo hatujamfanyia
uchunguzi na kubaini ni kitu gani kimesabisha kifo chake ingawa
anajeraha mdomoni na anavuja damu sikio la kushoto'alisema Daktari huyo
Akizungumza na Mtandao huu nje ya Zahanati hiyo Baba mdogo wa
marehemu huyo Bw Salum Hussein Mnyika[69] alidai kwamba kwa kipindi
kirefu mwanaye huyo alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo mkubwa.
"Mwanangu ni mkazi wa kijiji hicho cha Mwabwegele kinachogombaniwa
hivyo leo asubuhi alijumuika na wenzake kwenye maandamo hayo ya kufunga
barabara na kwamba alitoka kwenye kijiji hicho kwa kutumia usafiri wake
wa baiskeli mpaka nyumbani kwangu ambapo aliichacha baiskeli na kwenda
kujumuika nawakulima wenzake, majira ya saa sita nilijulishwa kwamba
mwanangu huyo amefariki,tunahisi huenda mstuko ule wa mabomu umestua
moyo wake na kusababisha kifo hicho"alisema Bw Mnyika.
| Wananchi wakiwa nje ya Zahanati ya Dumila kwa lengo la kuwapa pole wenzao waliojeruhiwa kwenye vurugu hizo. |
| Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kilosa eneo la Dumila. |
| Wananchi wa wilaya ya Kilosa ambao wengi wao walikuwa ni wakulima wakimsikiliza Mkuu huyo wa Mkoa. |
| Mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akizungumza na kamti hiyo nje ya kituo cha polisi Dumila kabla ya kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Kilosa leo mchYaliyotokea Dumila, Morogoro |
No comments:
Post a Comment