Sintofahamu bado inazidi kuitesa mtwara. Vurugu zimeendelea tangu asubuhi saa tatu leo tarehe 25.01.2013.
kituo kimoja cha polisi chateketezwa kwa moto, mwandishi wa Channel Ten amejeruhiwa na polisi na kushonwa nyuzi saba pamoja na gari la polisi kuharibiwa na mawe. Hali ni tete.
Pia inasemekana nyumba ya Hawa Ghasia imevunjwa na wananchi pamoja na nyumba ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mtwara.
Kwa upande mwingine inasemekana polisi wameingia kwenye nyumba ya mwanajeshi na kumtoa na kumpa kichapo kitendo kilicho mlazimu mwanajeshi huyo kupiga simu na kuwaita wenzake na kinachoendelea ni mpambano kati ya polisi na wanajeshi.
(Kutoka mitandao ya kijamii)
No comments:
Post a Comment