Jana wanafunzi hao walikuwa katika jimbo la Kilolo (kwa Profesa Msolla) katika kijiji cha Lundamatwe.
Kero kubwa inayowakumba wanakijiji hao ni uporwaji wa ardhi zao unaosimamiwa na mwenyekiti pamoja na mtendaji wa kijiji hicho,wajane wamekuwa ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo kwani itokeapo wamefiwa na waume zao basi hunyang'anywa ardhi na wakitaka kudai hupigwa na kutishiwa kupelekwa mahakamani.
Wanafunzi walipata kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi hao juu ya sheria ya ardhi ambayo inaonekana kutokujulikana kabisa kwao,pia waliwataka wananchi hao kuzifahamu haki zao za msingi katika jamii ikiwa ni pamoja na kudai kujua mapato na matumizi ya fedha zao kila ifikapo kipindi cha miezi mitatu
Mafanikio ya mkutano huo yalikuwa ni makubwa kwani baada ya elimu ile kuna wazee walijitokeza na kurudisha kadi za CCM kwa madai kuwa hawakujua namna ambavyo wamekuwa wakinyanyaswa na kuonewa na watawala hao
MATUKIO KATIKA PICHA
Mwenyekiti wa tawi Rose Mayemba akitutubia wananchi wa kijiji cha Lundamatwe
Katibu wa tawi Nicolaus Francis akiwahutubia wananchi
Kamanda Frank Malata akihutubia wananchi wa kijij cha Lundamatwe
Kamanda Gody Maganga akihutubia wananchi wa kijiji cha Lundamatwe
Makamanda wakiwa katika pozi kijiji cha Lundamatwe
Kada mkongwe wa CCM akitoa sababu za kukihama chama hicho
No comments:
Post a Comment