Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Saturday, January 19, 2013

WANAFUNZI IRINGA MJINI WAENDELEA KUHAMASISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (chadema) kiko katika mpango wa kutunza mazingira wakianzia kwenye jimbo la Iringa mjini.Kazi hii ilianza kufanyika kuanzia wiki iliyopita ambapo Mbunge wa jimbo hilo(Mch Peter Msigwa) akiwa na wananchi wa Iringa alifanikiwa kwa kiwango kikubwa kuzoa taka na kusafisha mifereji ndani ya manispaa.

Katika mwendelezo huo leo wanafunzi wa chuo kikuu cha RUCO walikuwa wanafanya usafi katika makaburi ya Mlandege,lakini pia walipanda miti katika bustani ya manispaa ambayo iko posta.

Wanafunzi wamewaomba wananchi wawe mstari wa mbele kuufanya mkoa wao kuwa safi bila kujali hilo ni jukumu la nani hasa kiutaratibu kwani madhara huwakuta woye bila kujali nani alistahili


HAWA NI WANAFUNZI WA RUCO KATIKA MATUKIO MBALIMBALI




wanafunzi wa RUCO wakisukuma mkokoteni wenye miti tayari kwa kwenda kupandwa
katibu wa tawi la RUCO bwana Nicolaus Mpandula(mwenye skaf) akishiriki kupanda miti



wanachama wa CHADEMA RUCO wakifukua shimo tayari kwa kupanda mti





Mwenyekiti wa tawi la RUCO(Rose Mayemba) akifyeka nyasi katika makaburi ya Mlandege









Wanachama wa RUCO baada ya zoezi la kufyeka nyasi katika makaburi ya mlandege

No comments:

Post a Comment