Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba jioni ya leo, Mh. Job Ndugai amelazimika kuahilisha bunge kutokana na wabunge wa upinzani kusimama wote kwa pamoja kupinga undeshaji wake mbovu wa shughuli za bunge. Hii ilitokana na yeye kutaka kuondoa hoja binafsi ya Mh. John Mnyika.
Itakumbukwa ya kwamba hivi karibuni, bwana Ndugai alizua tafrani pale alipotaka kumlazimisha Mh. James Mbatia kukamilisha hoja yake binafsi iliyohusu mitaala ya elimu, bila kuwa ametimiziwa ahadi yake ya kupewa nakala ya mitaala hiyo, ndipo amalizie hoja.
Matumbo kwanza, uzalendo baadae. Yawezekana hii ndio
slogan mpya ya naibu spika Job Ndugai.
 |
| Hapa Mh. Ndugai akitoa miongozo kama ilivyo kawaida yake. |
 |
| Hapa Mh. Myika akijitahidi kuwasilisha hoja yake juu ya kuboreshwa kwa upatikanaji wa juduma ya maji safi na ushughulikiaji wa maji taka jijini Dar es Salaam |
 |
| Baada ya kuona Mh. Ndugai haeleweki, wabunge wakaamua kusimama ili kuonyesha kutoridhishwa kwao na bwana Job. |
 |
Wabunge wa upinzani wakitoka nje ya ukumbi wa bunge siku mbili zilizopita kutokana na miongozo ya Mh. Ndugai
|
WHO CARES?
No comments:
Post a Comment