Juma lililopita, Tanzania ilipokea ugeni kutoka Democratic Repubic of Congo uliokuwa ukiongozwa na Rais Laurent Kabila. Bila shaka kama ilivyo desturi ya ujio kama huo, ulikuwa ni wa kitaifa. Ujio huo unadhihirisha ni jinsi gani viongozi wa Afrika walivyokua mbali ya uhalisia [out of touch with reality].
Viongozi wengi hujinadi juu ya ufahamu wao wa hali ngumu ya kimaisha barani na hupenda wafahamike kama watu ambao wapo kwa ajili ya maslahi ya watu masikini ambao ndio wachaguzi wao. Kwa mtizamo wa karibu zaidi, mtu huweza kubani kuwa wengi wao kama si wote ni waongo [simply liars]. Huwezi kushuhudia juhudi za dhati za kutaka kuwakomboa watu wao kimaisha miongoni mwa viongozi hawa. Tizama vipaumbele vyao.
Katika hali ya kawaida, tungetaraji kuona viongozi wa bara la Afrika wakiwa wapole [humble] ili kuelezea aina ya maisha wanayoishi watu wao. Hata hivyo ni tofauti. Wanafundisha maji na kunywa mvinyo. Hii hujidhihirisha kupitia maisha ya anasa na undumilakuwili [hypocrisy] ambayo watawala hawa wanakuwa wamejichagulia. Pichani, ni baadhi tu ya 'midoli' ya watawala wa kiafrika.
No comments:
Post a Comment