Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Monday, February 4, 2013

Vurugu CCM Vs. CHADEMA mkoani Dodoma

Kwa mujibu wa magazeti na vyombo mbali mbali vya habari nchini, sherehe za CCM za kuazimisha miaka 36 toka kuanzishwa kwake ziliingia dosari kutokana na tafrani iliyo ibuka kati ya wafuasi wa Chadema na wale wa CCM mkoani Dodoma.

Zogo kuu lilitokana na suala la kupandishwa ama kutokupandishwa kwa bendera. Wafuasi wa CHADEMA walifika eneo ambalo sherehe za CCM zilikuwa zikifanyika na kutaka kupandisha bendera ya chama chao katika nafasi [spot] ambayo bendera hiyo ilikuwepo tangu awali, ila ilishushwa na watu wanao sadikika kuwa ni wafuasi wa CCM, ambapo walichukua fursa hiyo kusimika ya kwao. 

Kwa kifupi kabisa, ni tofauti hiyo ndiyo iliyozua tafrani. Wakati hayo yakitokea, kiongozi wa CCM, Ismail Aden Rage ambaye pia ni mbunge wa Tabora, alikuwepo na cha kushangaza, alishiriki kikamilifu katika kutoa adhabu kwa wapinzani wao kama picha hapo chini zinavyo onyesha.

Je, wafuasi wa CHADEMA hawakuweza kuvuta subira na kuwa wavumilivu [tolerant] na kuhakikisha  kwamba shughuli za CCM zimekamilika nao kuweza kutimiza azma yao ya kupandisha hiyo bendera yao? Kulikuwa na ulazima gani wa wao kujitokeza wakiwa katika 'sare' zao eneo lililo tapakaa kijani, njano na nyeusi?

Ismail Aden Rage mheshimiwa, ni "kiongozi" ambaye amepitia misukosuko mingi ya kijamii. Itakumbukwa kuwa bwana Rage alikutwa na hatia ya kutembea na bastola yake huku akiwa ameining'niniza kama simu wakati wa uchaguzi mdogo kule Igunga. 

Picha zilizopatikana katika mitandao mbali mbali ya kijamii zinaonyesha ni jinsi gani mheshimiwa huyo alivyokuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wafuasi wa CCM wanajichukulia sheria mkononi na kuwaadhibu wapinzani wao kutoka chadema.

Ufike muda wanajamii wajifunze kuwa na uvumilivu wa kisiasa na kuepukana na mazingira ambayo yanaweza kupelekea fujo. Vitendo vya mheshimiwa vinazidi kudhihirisha ni jinsi gani watanzania tulivyokuwa na "mkosi" katika suala zima la kiutawala. 

Hapa bwana Ismail Aden Rage akiwa na silaha iliyo mponza katika uchaguzi wa Igunga

Ismail Aden Rage akiwa na mti alioutumia "kutoa hukumu"

Hapa Ismail Aden Rage [mwenye kofia ya njano] anaonekana akidhibiti 'kitoweo'. WAPI UONGOZI?

Mfuasi wa CHADEMA akiandamwa na wafuasi wa CCM kwa mawe. Kulia mwisho, 'baba' kabeba jiwe mithili ya mtu aliyeona nyoka. Mwenye bahasha anaonekana akifurahia tukio huku naye 'akituma' jiwe kumfariji kijana wa CHADEMA.
"Chukua hiyo". Ndivyo anavyo onekana kusema anayerusha teke. 


No comments:

Post a Comment