[kutuka mitandao ya kijamii]
Kabla ya kuhitimisha hoja binafsi, Mh. James Mbatia aliitaka serikali kupitia kwa waziri mkuu kuwasilisha mitaala ya elimu nchini katika meza ya spika kama ilivyo ahidiwa, ndipo ahitimishe hoja yake.
Kutokana na kushindwa kufanya hivyo, Naibu spika Job Ndugai kama ambavyo ingetarajiwa, alilazimika kuikingia kifua serikali kwa kumuamulu Mh. Mbatia kuhitimisha hoja yake kwani yeye ndiye mwenye maamuzi ya kuitaka serikali kuwasilisha au la.
Katika jitihada zake za kukatiza hoja ya Mh. Mbatia, ndugu Ndugai alitoa nafasi kwa Mh. Hamis Kigwangala kuwasilisha hoja yake, jambo lililomfanya Mh. Mbatia kutoka nje ya ukumbi wa bunge huku akifuatwa na wabunge wengine wa upinzani.
No comments:
Post a Comment