Katika hali ya kusikitisha na kushangaza Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameliambia bunge jioni hii kwamba serikali ya CCM imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.
Nchimbi amesema hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa.Waziri amesema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.
Hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Ikumbukwe ni hapo jana tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali ya CCM wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kukidhibiti Chadema na kukiimarisha CCM.
source jf
No comments:
Post a Comment