Kwanza
namshukuru MUNGU wa mbinguni kwa kuwa mwaminifu kwetu tangu wakati wa
kuanza mchakato wa uchaguzi hadi kupatikana kwa ushindi.
Lakini pia niwashukuru wanafunzi wote waliotupigia kura na wasiotupigia
kwa maombi yao ya usiku na mchana hadi tumeibuka kidedea katika uchaguzi
huo ambao ulikuwa ni wa kihistoria
Haikuwa kazi rahisi kama inavyoweza kudhaniwa bali ilikuwa ni safari
iliyojaa fitina,majungu,unafiki huku ikitawaliwa na wimbi kuu la
USALITI.
Wenzetu wengi walijitenga nasi huku wakiinua vikwazo mbalimbali, wengine
walisema tunatembea na bendera za vyama,wengine wakasema tumetumia
mavazi ya chama, na hata wengine wakadiriki kusema kuna kiongozi mkubwa
wa chama alishiriki nasi kupanga namna ya kumpata Rais.
Lakini sisi tunakiri kwamba kama si NGUVU YA UMMA, iliyotuamini na
kutusikiliza na hatimaye kutupa ridhaa sisi hatukuwa chochote katikati
ya wana wa RUCO,yote yaliyosemwa na fitina zote zilizofanywa ilikuwa ni
mpango wa makusudi kabisa wa watu fulani kutugawa sisi watoto wa baba
mmoja.
Leo tarehe 20/05/2013 mnamo saa 8:16 za usiku alitangazwa bwana MSANGI
RUSTON kuwa Rais halali wa chuo kikuu cha RUCO na Bi FLORAH YOHANA kuwa
makamo wa Rais kwa mwaka wa masomo 2013/2014
Ikumbukwe kuwa mwaka jana wakati wa uchaguzi vurugu kubwa zilitokea
baada ya Mkuu wa Mkoa kutoa vitisho kwa baadhi ya wajumbe wa tume na
wengine kupewa amri ya kujitoa ili wampitishe mgombea ambaye lilikuwa
chaguo lake
SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU

No comments:
Post a Comment