Mama Mmoja Mjamzito Mkazi wa Kijiji Cha Itunduma Wilayani Njombe Jestina Zabron Mhema Miaka 23 Amepotea Katika Mazingira ya Kutatanisha,Akiwa Katika Hospitali ya Kibena Mjini Njombe Wakati Akisubiri Kujifungua.
Aidha Kutokana na Tukio Hilo Wananchi wa Kijiji Hicho Wameiomba Serikali Kuimarisha Ulinzi Hospitalini Hapo Ili Kuzuia Matukio Kama Hayo Yasiweze Kujitokeza Kwa Mara Nyingine Tena Katika Hospitali Hiyo.
Wakizungumza na mwandishi wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com Kwa Masikitiko Makubwa Hospitalini Hapo Wananchi wa Kijiji Hicho,Pamoja na Kushangazwa na Tukio Hilo Pia Wameelezea Masikitiko Yao Juu ya Tukio Hilo na Kusema Uongozi wa Hospitali Unapaswa Kuwa Makini Katika Ulinzi na Namna ya Kuwalinda Wagonjwa.
Yustin Nyagawa ni Mwenyekiti wa Kijiji Cha Itunduma na Pasval Kaduma ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kibena Hospitali Wanawaomba Wananchi Kushirikiana Ili Kuweza Kumtafuta Mama Huyo Kwa Kuwa Taarifa za Awali Zinaonesha Kuwa Hakuna na Matatizo ya Akili Hivyo Huenda Amepotea Katika Maeneo ya Jirani na Hospitali Hiyo.
Imedaiwa Kuwa Mama Huyo Alipotea May 26 Mwaka Huu Majira ya Saa sita Mchana Baada ya Kukaa Hospitalini Kwa Zaidi ya Wiki Moja Sasa Akisubiri Kujifungua.
Huyu ndiye Mama aliyepotea Jestina Zabron Mhema Miaka 23 katika Hospitali ya Mji Njombe Kibena may 26 mwaka Huu.
Maandamano Yafanyika kumtafuta kibena Hospitali.
Wakazi wa Itunduma Mtwango wanaelekea
kumtafuta Mama huyo aliyetoweka katika Mazingira ya Kutatanisha akiwa
katika Hospitali ya Kibena.
No comments:
Post a Comment