Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Wednesday, May 29, 2013

MAUAJI YA KAMANDA BARLOW..SIRI NZITO YAJICHUKA,WABUNGE,VIONGOZI WA JUU WA SERIKALI KUHUSIKA


Kijana Mohamed Malele aliyejisalimisha kwenye vyombo vya ulinzi na usalama akijitambulisha kuwa mshirika wa mtandao uliohusika kumuua kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, amepewa hifadhi maalum na IGP wa polisi Said Mwema.

Chanzo cha habari hizi kimenasa taarifa kwamba malele anahifadhiwa ktk nyumba maalum jijini Dar es Salaam akilindwa na polisi wenye silaha na kupewa huduma zote za kibinadamu.

Malele ana siri nzito juu ya mtandao mpana wa mauaji ndani ya jeshi la polisi unaohusisha watumishi wengine kutoka vyombo vya ulinzi na usalama, wafanya biashara na wanasiasa.

Habari za karibuni kabisa zinasema kwenye mtandao wa uhalifu wamo wabunge na naibu waziri.  

Mtandao huo unatajwa na malele ambaye ni mkazi wa kijiji cha Igoma, Kwimba Mwanza, kuwa ndio uliohusika na mauaji ya kamanda Barlow usiku wa kuamkia octoba 13 mwaka jana ktk eneo la Kitangiri jijini mwanza, alipokuwa anamrejesha mwalimu anayetajwa kwa jina la Doroth Moses, aliyekuwa naye ktk kikao cha harusi.

Malele alikamatwa ijumaa may 10, mwaka huu alipokuwa ktk Lango la Bunge mjini Dodoma wakati akitafuta wabunge kadhaa.

Malele anatajwa kuwa mtu muhimu ambaye taarifa zake zinawasaidia viongozi wa juu wa vyombo vya ulinzi na usalama na serikali kwa ujumla kutambua na kuufumua mtandao wa uhalifu ndani ya Jeshi la polisi
 

source..jf









 

source...jf 

No comments:

Post a Comment