Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Sunday, June 23, 2013

MNYIKA: MWIGULU NCHEMBA, ADVOCATE NYOMBI WANAWATUMIA VIJANA KAMA CHAMBO, LENGO NI KUWAMALIZA VIONGOZI WA JUU WA CHAMA

Tangu tulipoanza mchakato wa chaguzi ndogo za madiwani  kulikuwa na machafuko karibu kila kona ya Tanzania. Tumeshuhudia mabomu yakilipuliwa mkoani mbeya, kuumizwa vibaya kwa viongozi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari, lakini pia tumeshuhudia damu ya wenzetu ikiililia ardhi huko jijini Arusha, tukio ambalo limesisimua hisia za wengi si Tanzania tu bali dunia nzima kwa ujumla.

Matukio haya yanafanya akili za wengi kufanya rejea, matukio mangapi yametokea na ni kwanini yatokee ili ikiwezekana yapatiwe ufumbuzi wa haraka kuliko kuendelea kutishia uhai wa mwananchi anayelindwa kikatiba  ikiwa ni pamoja ha haki ya msingi ya binadamu kuishi.

Leo CHADEMA walikuwa na kikao makao makuu ya chama jijini Dar-es-salaamu kujadili juu ya mambo haya, kikao hiki kiliongozwa na mhe J.J. Mnyika akiwa na  prof Abdalah Safari.

Mhe mnyika alikuwa na haya ya kusema:

Njama hizi ni za kisiasa na zimepangwa kwa vikao mbalimbali kwa mujibu wa taarifa zao walizonazo. Anasema vinara wa mkakati huu ni Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu CCM Bara na Advocate Nyombi Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi. Anasema lengo la kuwakamata vijana hawa ni kama chambo tu lakini wanaotafutwa ni viongozi wakuu wa Chama. Mnyika anasema alikamatwa kijana Evodius tarehe 2, Aprili huko kagera na wakamweka mahabusu siku 3 bila dhamana, akapelekwa Mwanza nako akaa mahabusu siku 4, wakamsafirisha kwa ndege kuja Dar es salaam. Muda wote akiwa mikononi mwa jeshi la Polisi alipigwa sana na akiwa Dar es salaam alipelekwa Makao Makuu na kufungiwa ndani akiwa na Advocate Nyombi na hapo aliteswa kwa shoti ya umeme sehemu za siri wakimlazimisha akiri kwa kuandika maelezo kuwa waliohusika na tukio la tindikali ni Mbowe, Slaa, Mnyika na Tundu Lissu.


Source-kurugenzi ya habari CHADEMA

No comments:

Post a Comment