Lango kuu la kuingia Ikulu (Picha zote kwa hisani ya Michuzi)
Rais akiwasalimia wananchi waliopo hapo Ikulu kumlaki Obama.
Upande wa Mashariki -Obama Avenue (Zamani Ocean Rd )-
Jumba jeupe la Kibongo (Ikulu)
MAANDALIZI YA MAPOKEZI YA OBAMA YAKAMILIKA, TASWIRA ZA IKULU ASUBUHI HII
Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda mswano, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.
Bendera zikiwa zimepangwa na kupangika katika upande wa lango kuu la Mashariki,Ikulu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama.
Jengo la Ikulu.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akisoma ratiba.
No comments:
Post a Comment