Katika hali ya kusikitisha watu saba mkoani Mbeya, jimbo la Rungwe Mashariki, kata ya Kiwira, vijana saba wamejikuta wakisota rumande baada ya kupinga bajeti ya kijiji iliyopendekezwa. Vijana hao ni pamoja na diwani Laurent Albert Mwakalibule, Michael Simon, Gwamaka Mfaume, Simon Mwasakyeni, Gasper Msinga, Lwangalo Asajile, Bwigone Mwakipesile na Moses Sanga.
Hali hiyo iliwasibu mara baada ya kupinga bajeti iliyokuwa ikisomwa na mtendaji wa kijiji aliyefahamika kwa jina la Andrew Mwakasaka kutokana na malalamiko ya muda mrefu ya utunzaji na uwasilishwaji mbovu wa mapato na matumizi kwa wananchi. Wananchi hao walikuwa wakihoji kuondolewa kwa mfumo bora zaidi uliokuwepo hapo awali uliohusisha fomu zilizofahamika kama HW5 na badala yake kuwekwa mfumo wa risiti ambazo hazichanganui miamala vizuri.
Zaidi wananchi hao walikuwa wakihoji juu ya kutokufuatwa kwa utaratibu uliozoeleka ambapo mara baada ya mapato yatokanayo na shughuli mbali mbali za eneo kukusanywa na kuwasiliswha halmashauri, kuna asilimia ambayo inapaswa irudi kwenye kijiji kwa shughuli za maendeleo jambo ambalo halikuwa limefanyika tangu mwaka 2010.
Kutokana na hali hii, ndipo wanakijiji walipoamuru ofisi ya kijiji ifungwe mpaka hapo mtendaji atakapojibu hoja zao. Hata hivyo kibao kiliwageuka wanakijiji hao baada ya baadhi yao kukamatwa na polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya bwana Chrispine Meela wakemo watajwa hapo mwanzo. Watu hao walifunguliwa shitaka la kumzuia mkurugenzi kufanya kazi kwenye soko la kijiji kwa madai eti walichochea kufungwa kwa ofisi ya mtendaji.
Jambo la kustaajabisha kabisa katika mchakato mzima wa vijana hawa saba pamoja na diwani wao kukamatwa, ni namna ambavyo utambuzi ulikuwa wa kibaguzi. Katika tukio ambalo lilihusisha wanakijiji kupinga mwenendo wa uendeshwaji wa shughuli zinazohusu maendeleo yao, iweje watambuliwe wachache na kufunguliwa mashitaka?. Diwani huyo wa kata ya kiwira bwana Laulent Abel Mwakalibule(CHADEMA) ambaye alifunguliwa kesi ya kuhamasisha watu kuigomea bajeti hiyo ya kijiji ambayo ndio sababu ya kufungwa kwa ofisi hiyo yeye yuko huru kwa dhamana.
Washtakiwa hao ambao awali hakimu aliwatangazia kuwa dhamana zao ziko wazi baada ya kutimiza masharti yote waliyopewa waliombiwa dhamana imefungwa hadi hapo tarehe16/07/2013. itakapojadiliwa upya
Siku ya tarehe 1 mwezi Julai walipo kamatwa walifikiswha mahakamani kesho yake na diwani kufanikiwa kupata dhamana huku wale vijana wengine
No comments:
Post a Comment