Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameeleza sababu za Tume hiyo kupendekeza Serikali tatu, huku akisisitiza kuwa suala hilo lilikuwepo tangu siku nyingi. Kauli hiyo inaonekana kama kukijibu Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimependekeza kuwepo kwa Serikali mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari Warioba aliongeza,
“Mikutano na Mabaraza ya Katiba siyo ya kupiga kura bali ni kujadili na kutoa hoja ambazo zitakuwa na msingi kwa masilahi ya taifa na siyo kutetea masilahi ya kundi au watu fulani,”
CCM
Tangu rasimu hiyo ilipotolewa mapema Juni mwaka huu, chama hicho kilionyesha kutokuridhishwa na rasimu hiyo na kuahidi kuipeleka kwa wanachama wake.
Katika kuonyesha kutokuridhshwa huko, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaeleza wajumbe wa Mabaraza ya Katiba jijini Dar es Salaam juzi azma ya chama hicho kuwa na rasimu mbadala.
Nape ambaye aliitumia siku nzima ya Alhamisi kuzungumza na wajumbe hao wa mabaraza, alisema wameandaa rasimu yao ambayo imeandikwa vitu wanavyohitaji na wanachama wote wanapaswa kuvisimamia.
==Mwananchi==
No comments:
Post a Comment