Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Sunday, August 18, 2013

KATA KWA KATA YAIMALIZA CCM NJOMBE



Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Mkoani Njombe kimeanza mikutano yake ya kata kwa kata kwa lengo la kujenga chama ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wake.

Chama hicho ambacho kimeanza shughuli zake rasmi wiki iliyopita pia kupitia mikutano hiyo ina elimisha wananchi hao namna ya kuipata katiba mpya ambayo itazingatia matakwa na mahitaji yao na si matakwa ya wachache wenye nia ya kulihujumu Taifa.

Hatua hii imekuwa ni msumari mkali sana kwa chama cha Mapinduzi(CCM) ambao wamekuwa wakihaha huku na huko ili kuzuia watu wasihudhurie mikutano hiyo kwa kuhofia wananchi kukihama chama chao hivyo kuwahonga vijicent kidogo huku wengine wakitishiwa kufukuzwa kwenye vibanda vyao vya biashara.



 Wakitoa kero zao wanawake wa kata hiyo kwa mgeni rasmi ambaye pia ni katibu CHADEMA wa wilaya ya Njombe Bwana Alatanga Nyagawa, wanawake hao walisema ni miaka mingi sasa wanahangaika na suala la maji japo swala hilo lilikuwa ni sehemu ya ahadi ya Mbunge wao Mh Deo Sanga ali maarufu kama JAH PEOPLE.

Wananchi hawa ambao pia wapo kwenye mchakato wa kupeleka mawazo yao kwenye mabaraza ya katiba wanausubiri kwa hamu ujio wa Mwenyekiti wa chama Mhe MBOWE akiambatana na Mhe John Mnyika pamoja na Mhe Tundu Lissu ambao wanatarajia kuhutubia mjini hapo tare 22/08 siku ya alhamis wiki ijao



Jana Jumamosi CHADEMA walikuwa katika kata ya UBENA katika mji wa makambako.


Katibu wa wilaya ya njombe Alatanga Nyagawa akihutubia mkutano huo.






Mwenyekiti wa jimbo jimbo la njombe kaskazini akihutubia

Katibu wa jimbo la Njombe Kaskazini bwana Bennedict kyando akihutubia

Mhazini wa jimbo la njombe kusini bwana Kazimoto Edward akihutubia



Mkufunzi ngazi ya msingi  jimbo la Njombe Kusini bwana Emmanuel Kayombo akuhutubia katika mkutano huo
 Rose Mayemba( mwenyekiti wa zamani chuo kikuu cha RUCO-CHADEMA) akihutubia wananchi wa kata ya Ubena

Sehemu ya wakazi wa Ubena  waliohudhuria mkutano huo.



No comments:

Post a Comment