Wananchi wa kata hiyo iliyoko wilaya ya mufindi mkoani Iringa waliamua kwa pamoja kujenga mnara katika eneo hilo ili kutokupoteza tukio hilo la kihistoria ambalo liliihuzunisha dunia nzima.Mnara huo ambao umejengwa kwa gharama ya fedha za kitanzania zisizopungua mil mbili umeonyesha kuwasisimua sana wakazi wa eneo hilo pamoja na maeneo mbalimbali ambapo kila aliykuwa akiangalia mnara huo hakusita kutoa machozi ya majonzi na uchungu mkali
katika uzinduzi wa mnara huu pia alishiriki mdogo wa marehemu Mwangosi ambaye aliwashukuru sana Chadema kwa kushirikiana nao kuanzia mwanzo wa msiba mpaka sasa ambapo bado wanaendelea kuiangalia ile familia kwa karibu sana, Pia amewaasa waandishi wa habari wanaoandika uongo juu ya familia ya marehemu iliwemo kuipakazia chadema kuwa imeitelekeza familia hiyo, pamoja ha hayo pia amepinga habari inayosema kuwa mmoja kati ya watoto wa marehemu anasomeshwa na serikali kwani wao ndio wanaojua watoto wako wapi na wanasomaje.
Pamoja na vitisho vingi kutoka kwa polisi ambao taarifa zinaonyesha walianza kuzunguka maeneo hayo kuanzia saa kumi za usiku mpaka wakati wa tukio lenyewe wananchi hao waliokata tamaa na serikali yao hawakusita kusogea eneo la tukio japo wengi wao walionyesha kuwa waoga na wengine kukaa mbali kabisa na tukio ili kuepuka kilichomkuta mwanahabari huyo mwaka katika eneo hilo.
Gari za polisi zisizopungua tatu zilikuwa zikiranda maeneo hayo huku askari wengine wakiwa wamezagaa maeneo mengi ya mji huo hali iliyopelekea kutanda kwa hofu na mashaka miongoni mwa wengi waliokusudia kuhudhuria uzinduzi wa mnara huo ambao ulizinguliwa na naibu katibu mkuu wa CHADEMA -zanzibar bwana Hamad Yusuf akiwa ameongozana na Benson Kigaira
Daudi Mwangosi likuwa na mwandishi na mpiga picha wa kituo cha television cha channel Ten na pia Mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa iringa alikufa tarehe 2/09/2012 kwa kulipuliwa na bomu na polisi wakati wa ufunguzi wa M4C mkoa wa Iringa
Makamanda wa Chadema wakiwasiri eneo la mnara wa Daudi Mwangosi.
Huu ndio mnara uliojengwa na wananchi maeneo alipofia Daudi Mwangosi.
Naibu katibu mkuu Chadema akizundua mnara wa Daudi Mwangosi.
kuanzia kulia ni Benson Kigaira,mdogo wa daudi mwangosi,mama aliyenusurika kifo wakati polisi wakilipua mabomu,Naibu katibu mkuu zanzibar, mwenyekiti wa kanda kusini...
huyu ni mmoja kati ya walionusurika kifo wakati polisi walipokuwa wakilpua mabomu
Sehemu ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa mnara huo.
huu ni mwili wa marehemu daudi mwangosi baada ya kutawanywa kwa bomu na jesh la polisi
Daud mwangosi (katikati ) enzi za uhai wake


No comments:
Post a Comment