Ni yule aliyepiga picha na Mh. Godbless Lema huku akionyesha alama ya vidole viwili itumikayo na CHADEMA. Jeshi la Wananchi Tanzania limetoa tamko kuwa linafanya upelelezi kubaini kama kweli kijana yule ni askari wa jeshi hilo na endapo itabainika kuwa hivyo, moja ya hatua zitakazo chukuliwa ni kumfukuza kazi mara moja. Hii ni kutokana na kuwa askari wa jeshi hilo kama ilivyo kwa vyombo vingine vya usalama, hawaruhusiwi kujihusisha na siasa moja kwa moja.
Hata hivyo kijana husika akiwasiliana na gazeti la Mwananchi amesema yuko tayari kufukuzwa kazi, ila si kunyimwa uhuru wa kuishabikia CHADEMA.
No comments:
Post a Comment