Baada ya kiboko ya mkapa kutoa vionjo vyake kwa wanairinga{vincent nyerere}, mnadhimu mkuu kambi ya upinzani bungeni Mh. Tundu Lisu atahutubia wakazi wa Iringa mjini siku ya Alhamisi tarehe 03.01.13 katika viwanja vya Mwembetogwa, Manispaa ya Iringa mjini.
Ni ukweli usiopingika kwamba wakazi wa iringa wana hamu kubwa ya kumsikia kamanda huyo baada ya kufanikisha kwa kiwango kikubwa ushindi wa rufaa ya kesi ya Mh. Godbless Lema iliyomrudishia ubunge wake mapema wiki iliyopita.
Tundu lisu ni mbunge wa jimbo la Singida Mashariki
Mh. Tundu Lisu akiwa na Mh. Peter Msigwa siku alipotembelea mjini iringa
No comments:
Post a Comment