Baada ya mahakama kumrudishia ubunge Mh. Godbless Lema ambaye ni mbunge wa Arusha mjini siku chache zilizopita, baadhi ya wanasheria wametofautiana juu ya hukumu hiyo.
Mwanazuoni aliyebobea katika sheria na mwenyekiti wa chama cha wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law society), Profesa Issa Shivji pamoja na wanasheria wengine wamesema kuwa sehemu ya hukumu ya lema haikuwa sahihi.
Habari kutoka kwenye moja ya mitandao ya kijamii zinasema mwanazuoni huyo anaishangaa mahakama kwa kuwanyima wapiga kura haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi. Pia amesema mahakama haikusimamia sheria bali ilitunga sheria ya kwake kinyume na ile iliyopo.
Lakini wakili wa Lema (Kimomogoro) amepingana na kauli mwanasheria huyo kwa kusema kuwa pengine hakupata nafasi ya kuipitia hukumu kwa umakini.
No comments:
Post a Comment