Mchungaji na mbunge wa jimbo la Iringa mjini, Mh. Peter Msigwa amesema anashangazwa na kitendo cha viongozi wa C.C.M kuancha kushughulikia kero za msingi za watu wa Iringa na kujinadi kwenye vyombo vya habari kuwa watalirudisha jimbo hilo mikononi mwao.
Amesema kuwa watu wa Iringa wana matatizo mengi ikiwemo njaa iliyokithiri, ambayo C.C.M walipaswa kushiriki kuyatatua lakini wamekazana kupiga kelelee za kulirudisha jimbo jambo ambalo linawanyima wananchi haki zao za msingi.
Akizungumza na moja ya gazeti ya kila siku amesema jimbo hili lilikuwa mikononi mwao miaka yote na hawakufanya kitu. Iweje leo waone kwamba watakua na msaada kwa wananchi hao?
Pia mchungaji amesisitiza kuwa C.C.M waache kujisumbua kwani wananchi wamemwamini na yeye ndo mbunge halali wa jimbo hilo.
Mh. Peter Msigwa akitimiza moja kati ya ahadi zake kwa vijana kwa kuandaa mashindano ya michezo.
No comments:
Post a Comment