Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Thursday, January 24, 2013

LEMA ASITISHA WANAFUNZI KUENDELEA KUSOMA KORONA SEKONDARI


Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema leo amesitisha wanafunzi wa shule ya Korona Secondari iliyoko kata Ongutoto wilaya ya Arusha. Korona inayopaswa kuwa na wanafunzi 1,200 lakini kwa sasa ni wanafunzi 139 tu wanaofika shuleni hapo na tuliowakuta ni 118 tu, huku kidato cha kwanza wakiwa 19 badala ya 400.

Lema alifikia maamzi hayo kwa kile alicho kiita ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kutembea km 13 huku wakikosa masomo, wanafunzi hao wakitoa ushuuda walisema wamekuwa wakija shuleni na kurudi bila kusomaWalimu hufika saa sita na kuondoka saa saba na nusu.Wanafunzi hufika saa tano na kuondoka nane.
Wanafunzi hawafundishwi na wakifundishwa hufundishwa kipindi kimoja cha dakika 30.Wazazi wanatoa michango kiasi cha TZS 72,000/= ya chakula kwa watoto wao lakini hawaja wahi kupata chakula chochote kwenye shule hiyo, 32,000/= ya sare lakini hawaja wahi kupewa sare, 5,000/= ya vitambulisho lakini hawajawahi kupewa vitambulisho.
Watoto wana kunywa maji ya mto Kijenge ambao kwa wanyeji wa kijenge/Arusha wana jua namna ulivyo mchofu mto huo. Hali hiyo imepelekea watoto 98 wame hamishwa na kupelekwa kwenye shule zilizoko manispaa ya jiji la Arusha wakati wizara walishasema shule hizo zimejaa lakini baadhi ya wazazi walitoa ushuuda kuwa kuna rushwa kubwa inayofanyika katika kuhamisha watoto kwani kama huna TZS 200.000/= huwezi kumhamisha mtoto ndiyo maana waliobaki ni watoto yatima ambao wazazi wao ama hawana uwezo huo wa kutoa kiasi hicho cha pesa au hawa thamini elimu ya watoto wao.
Baada ya lema kusitisha mwanafunzi haao kwenda kusoma korona alimkabidhi Diwani wa kata hiyo kwenda na watoto kwenye ofisi yake na atakuwa anakaa nao hapo mpka siku watakapo patiwa shule za kuhamia ambapo Lema alishauri kuwa kila shule iliyoko kwenye jimbo hilo ichukue wanafunzi angalau watano tu, kwa muda ambao shule hiyo itakuwa ikifanyiwa marekebisho na kubadilishwa iwe boarding kitu ambacho ilionekana ndiyo suruhu ya kudumu, mbunge huyo aliahidi kutoa tofari 3000, solar panel, na pampu ya kuvutia maji na atatoa iwapo wanao husika wataonyesha nia...

Name:  korona.gif
Views: 0
Size:  108.2 KB

Name:  korona2.gif
Views: 0
Size:  80.7 KB

Afisa elimu, Diwani, Mbunge, kaimu mkurugenzi na mwalimu mkuu wa shule ya Korona.
Name:  korona3.gif
Views: 0
Size:  90.4 KB

Wanafunzi wa Korona Secondari wakishangilia maamzi ya mbunge wa Arusha mjiniya kusitisha masomo kwenye shule hiyo..

No comments:

Post a Comment