Edwin Bliss C

Success does not mean the absence of failure; it means the attainment of ultimate objectves. It means winning the war, not every battle.

Kufanikiwa hakumaanishi kushinda kila jambo; kunamaanisha kufikia malengo. Kunamaanisha kushinda vita na sio kila pambano.

Saturday, January 19, 2013

MTWARA KIMENUKA

KUTOKA KWENYE CHANZO CHA HABARI:
HIVI NDIYO HALI ILIVYOKUWA IKIENDA....FUATILIA

Hali mjini hapa ni tete! Mabomu yanarindima mjini hapa kuwatawanya wananchi wanaojiandaa na mkutano mkubwa unaotarajiwa kufanyika mjini hapa kuhusu suala zima la gesi.

Chanzo cha mabomu hayo kupingwa ni baada ya umeme kukatika/kukatwa eneo panapotarajiwa kufanyika mkutano huo uwanja wa mashujaa mjini hapa na baada ya kuona hivyo wananchi wakaamua kuandamana kuelekea Tanesco kujua chanzo cha tatizo hilo la umeme na hali hiyo kupelekea polisi kuanza kuvurumisha mabomu ya machozi.

Ifahamike kwamba kumekuwa na mvua kubwa mjini hapa toka usiku wa leo ambayo inaweza ikawa chanzo cha kukatika kwa umeme huo (huu ni mtazamo wangu) ingawa inaweza ikawa hujuma pia.

Eneo nilipo umeme upo hali hii ya sintofahamu imepelekea huduma muhimu za kijamii kama maduka na soko kufungwa.

updates:
wakuu nimetoka kwenye mkutano umefanyika hapo mashujaa kiukweli sikuweza kuendelea kuwaletea live kutokana na hali ya mvua pale uwanjani. kifupi mkutano umehutubiwa na wazungumzaji kadhaa wakiwepo wasanii na wabunge, wasanii walikuwa ni Afande Sele na Kala pina kwa upande wabunge ni Magdalena Sakaya, Sulemani Bungala (Bwege) na Barwan, wazuinguzaji wengime walikuwa ni katani na mtatiro

wote kwa hakika wamezungumza mengi sana na wote wameungana na wanamtwara katika kuhakikisha rasilimali ya gesi inawanuifaisha watu wa mtwara na kusini kwa ujumla. kwa upande wa wasanii hakika afande sele amejitahidi sana kuongea kwa kujenga hoja. pamoja na kuwa na hali ya mvua wananchi hawakuondoka pale uwanjani.

 kwa kweli serikali isipuuze haya madai ya watu wa mtwara kwa mfano kwa jinsi inavyoonekana vijana wako tayari kwa lolote. Katika mkutano huo kumekusanywa saini za watu 26,000 na kuwatuma wabunge kupeleka bungeni madai yao. Mbunge wa Lindi mjini ameeleza mara baada ya mkutano huo  kuwa madai ya wana Mtwara na kusini yote watakutana lindi kwa maandamano makubwa yatakayo fanyika tarehe 23 februari mwaka huu hadi kieleweke

Lakini pia kulikuwa na jambo la kusikisha, kumetokea ajali pale njia panda ya kuelekea airport ya Mtwara gari lililokuwa linatokea tandahimba likiwa na wananchi limepata ajali na watu watatu kuumia nakupelekwa hosptali ya mkoa ligula na mmoja inaelezwa hali yake sinzuri anatakiwa kupelekwa muhimbili kwa matibabu zaidi, jambo ambalo lilimfanya bwana katani kuumba umati mkubwa uliohudhuria kutoa mchango kuwezesha safari hiyo na wananchi kuitikia jambo.



Click image for larger version. 

Name: SAM_0187.JPG 
Views: 0 
Size: 2.79 MB 
ID: 80032Click image for larger version. 

Name: SAM_0188.JPG 
Views: 0 
Size: 2.72 MB 
ID: 80033Click image for larger version. 

Name: Photo0138.jpg 
Views: 0 
Size: 461.9 KB 
ID: 80034Click image for larger version. 

Name: Photo0136.jpg 
Views: 0 
Size: 481.9 KB 
ID: 80035

No comments:

Post a Comment