Ikumbukwe kuwa hiki ni kilio cha muda mrefu cha wamachinga kutafutiwa eneo zuri na lililoandaliwa kitaalam kwa ajili ya shughuli zao kabla ya kuwaondoa mahali hapo ambapo ndipo chakula chao kinapopatikana
Machinga hao baada ya kuona serikali haisikilizi kilio cha waliamua kurudi eneo hilo bila kibali cha manispaa na ndipo jeshi la polisi lilipotumwa kwenda kuwaondoa kwa nguvu.
Mbunge wa jimbo hilo Mhe Peter Msigwa ambaye alionekana kupita eneo hilo ameitwa kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano na mpaka naingia mtandaoni sikuwa na taarifa zozote za kuachiwa.
Abiria na wapiga debe stendi kuu wakinawa maji baada ya
kupigwa mabomu na kumwagiwa maji ya kuwasha na askari wa FFU hapo jana
wananchi wakishaanga matairi yaliyochomwa barabarani na watu wenye hasira kali
mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwasili eneo la vurugu kabla ya kuanza kwa vurugu hizo
Mbunge Msigwa akiondoka eneo la mashine tatu
Machinga wakisukuma gari ya mbunge Msigwa
Polisi wakimfuatilia mbunge Msigwa kwa nyuma baada ya kufika eneo hilo bila kufanya biashara kama alivyoahidi
Polisi wakianza kufukuza wananchi eneo
No comments:
Post a Comment